Dina Marios |
Maisha haya kila mmoja anasafari yake namna atakavyo anza na namna atakamaliza ni
Mungu ndio anajua.Kwa mfano kuna mtu atamaliza chuo akiwa na miaka 20 ata
struggle kwa miaka 5 kupata kazi.Mwingine atamaliza akiwa na miaka 25 na
akapata kazi mapema tu baada ya kumaliza chuo.Mwingine anaweza kuolewa bikira
na kusubiri miaka 10 kupata mtoto..mwanamke mwingine alotoa mimba kibao huko
nyuma anaolewa na kushika ujauzito hapo hapo.Jamaa mmoja anakuwa MD katika
kampuni akiwa na miaka 38 na kufariki akiwa na miaka 56,jamaa mwingine anakuwa
MD akiwa na miaka 50 na anaishi mpaka miaka 90.